Waziri Lukuvi atoa wito kwa viongozi kuwahimiza wananchi kujiandikisha

DODOMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe William Lukuvi ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya siasa viongozi wa dini viongozi wa kimila na viongozi wengine kushirikiana katika kuhimiza wananchi kwenda kujiandikisha kwa sababu ni haki yao.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,John Mnyika akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi walipokutana katika Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika jijini Dodoma.

Wito huo umetolewa leo Oktoba 11,2024 wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama Siasa.

Ameeleza kwamba haki ya mtu kujiandikisha inabaki pale pale awe mwanachama wa chama cha siasa au bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika jijini Dodoma.

“Tukijumlisha wanachama wetu wote kuna watu wanabaki ambao hawako kwenye fungu lolote katika vyama hivi vya siasa 19, lakini bado tunao ushawishi wa kutumia sauti zetu kuhimiza wananchi wote wenye umri wa kujiandikisha wajiandikishe na hatimae watumie nafasi hiyo kupiga kura.

"Tunaowajibu kama viongozi wa vyama vya siasa kwa pamoja kuufanya uchaguzi huu uwe mzuri."
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ali Khatibu akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika jijini Dodoma.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Fransis Mutungi akizungumza wakati wakati wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha (UDP),Mhe. John Cheyo amesema,"Nadhani sisi kama wadau wa siasa tunayo nafasi kukubaliana kwa kuwa na kauli moja ya kusimamia uchaguzi kulingana na kanuni na sheria ambazo tumejiwekea.

“Tunadhamira ya kuwa na uchaguzi huru na haki kwa kila mmoja wetu na kama ilivyoelezwa na Waziri Lukuvi na hiyo ndiyo dhamira ya Mhe Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Mhe. Cheyo.
Viongozi wa Vyama vya Siasa katika picha wakifuatilia kwa umakini Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika jijini Dodoma.

Awali Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini amesema huu ni mkutano ambao umeandaliwa tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kujipanga katika maandalizi ya chaguzi zinazoendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news