DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 24, 2024 amekutana na Balozi wa Belarus nchini Tanzania Pavel Vziatkin, katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Majaliwa amemweleza Balozi Pavel kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Belarus katika Sekta za Madini, Afya, Utalii, Kilimo na Biashara kwa faida ya nchi zote mbili.