Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt.Samia kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA Tanzania

DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 17, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA, linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya Maonesho kwenye Kongamano hilo, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanasimamia ukuaji wa Sekta ya TEHAMA.
Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amewataka vijana kutumia fursa ya Uwekezaji unaofanya na Serikali katika sekta ya TEHAMA ili kukuza uchimi binafsi na Taifa kwa ujumla.
Kaulimbinu ya Kongamano hilo ni “Kutumia Uwezo wa Akili Mnemba na Robotiki kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news