Waziri Mkuu azindua bwalo na bweni Shule ya Sekondari Kibasila

DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na viwango vya ujenzi wa bweni na bwalo kwenye shule ya Sekondari ya Kibasila iliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 1.13.
Mhe. Majaliwa amesema hayo leo Jumamosi, Oktoba 5, 2024 alipozundua jengo hilo ambapo amewataka wote watakaolitumia jengo hilo walinde miundombinu yake ili litumike kwa muda mrefu.
Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia amedhamiria kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu kote nchini.
Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia wanafunzi wa kike 228 hasa wa kidato cha tano na sita kupata elimu bora katika mazingira ya karibu hivyo kusaidia kuongeza ufaulu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news