DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 27, 2024 ni mgeni rasmi katika Tamasha la Buhaya Buhaya Festival linalofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Lengo la tamasha hilo ni kutangaza na kutambulisha fursa za vivutio vya utalii na uwekezaji vinavyopatikana mkoani Kagera.
Aidha, Tamasha hilo pia linalotoa fursa ya kuenzi na kuendeleza mila na desturi za jamii ya Wahaya kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Kagera.