Waziri Mkuu mgeni rasmi Mkutano wa 10 wa Wadau wa Lishe

MWANZA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 03, 2024 anafunga mkutano wa Kumi wa Wadau wa Lishe unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza.
Lengo la mkutano huo ni kudumisha dhamira ya pamoja ya Serikali na wadau katika kuongeza msukumo na uwekezaji katika kutekeleza Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe ili kukabiliana na changamoto za utapiamlo katika jamii, na kupokea tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe nchini kwa mwaka uliopita.
Pia, mkutano huo umelenga kutoa fursa kwa wadau wa lishe kukutana, kujadiliana na kupata maelezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Kitaifa wa Lishe (2021/22 - 2025/26) uliouzinduliwa mwaka 2021.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni ”Kuchagiza Mchango Zaidi Wa Wadau Wa Kisekta Ili Kudumisha Matokeo Bora Ya Hali Ya Lishe Nchini Tanzania”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news