GEITA-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Oktoba 11, 2024 amewasili mji mdogo wa Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo atakuwa mgeni rasmi katika Siku ya Mwalimu Duniani kwa mwaka 2024.

Mheshimiwa Majaliwa amepokelewa na Mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe, ambaye ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko.