Waziri Othman ashiriki Mkutano wa Mawaziri wa Nchi Ndogo za CHOGM

APIA-Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Nchi Ndogo za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Small States Ministerial) unaoendelea Apia, Samoa.
Katika mkutano huo Tanzania ilichangia mjadala wa Mawaziri kuhusu umuhimu wa kushughulikia changamoto za kiuchumi zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi kwa nchi hizo ndogo ili kuziwezesha kunufaika na fedha za misaada ya kimaendeleo pamoja na mikopo nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu( SDGs).
Mkutano umekubaliana na pendekezo la kuanza utekelezaji wa mpango kazi wa nchi ndogo za JYM (Commonwealth Small States Programme of Action 2024 - 2026) unaoelekeza nguvu zaidi kwenye kusaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, kusaidia katika kipindi cha miaka miwili ijayo, kwa kuzingatia hatua ya hali ya hewa, nafuu ya madeni, na upatikanaji wa fedha kwaajili ya shughuli za kimaendeleo kwa miaka miwili ijayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news