Waziri Ridhiwani Kikwete ashiriki Mbio za Hisani kumbukizi ya Miaka 25 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere

MWANZA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Oktoba 12, 2024 ameshiriki katika mbio za hisani (Marathon) ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 25 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Aidha katika mbio hizo Mhe. Ridhiwani Kikwete aliambatana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus.
Mbio hizo za hisani zimeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizoanzia Igoma Mnara wa Kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere na kuishia Kisesa jijini Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news