Waziri Tax aongoza maadhimisho ya miaka 79 ya Umoja wa Mataifa (UN)

DAR-Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Tax tarehe 24 Oktoba, 2024 ameongoza maadhimsho ya miaka 79 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo katika baraba ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mhe. Dkt. Tax amesema Tanzania imekuwa mwanachama hai katika Umoja wa Mataifa kwa miaka 63 mpaka sasa na imenufaika na harakati za Umoja huo za kuchochea maendeleo ya Taifa ya kisekta, mikakati ya kudumisha amani na umoja na juhudi za kutetea haki za binadamu.

Mhe. Tax amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa kupitia program za ushirikiano katika sekta mbalimbali zikiwemo maji, elimu, sheria na haki za binadamu, utawala bora na ushiriki katika vikao mbalimbali vya Kamisheni vya Umoja wa Mataifa ambapo nchi wanachama hupewa nafasi ya kuwasilisha hoja zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi endapo kuna hitaji la kufanya hivyo.

“Nikiwa kama Waziri wa Ulinzi nitaendelea kuhakikisha kuwa Tanzania inashiriki katika Kamisheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa zinazolenga kudumisha amani barani Afrika na Duniani kwa ujumla, ili kuweza kuunganisha nguvu katika kutatua changamo zetu,”alifafanua Mhe. Tax.

Aidha Mhe. Tax amesema falsafa ya Mhe. Dkt Samia inayozingatia suala la kudumisha Amani, Umoja, Maendeleo na jitihada za kujenga nchi, ni mfano mzuri wa kuigwa duniani katika kuleta maendeleo na kukuza Uchumi.

Akizungumzia kuhusu madhimisho hayo Balozi Noel Kaganda, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ameeleza kuwa Umoja wa Mataifa umetoa mchango mkubwa katika kuunga mkono harakati za Tanzania kupata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961.

Aliongeza kusema kuwa Umoja wa Mataifa umeendelea kuiwezesha Tanzania katika utekelezaji wa sera za maendeleo kupitia mpango wa maendeleo wa miaka mitano na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Mark Bryan ameeleza kuwa Shirika hilo litaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali zinazolenga kuleta ustawi wa kijamii na kiuchumi.

Vilevile, amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Seriklai ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo zimeongeza ufanisi katika sekta mbalimbali ikiwemo eneo la Demokrasia na Utawala Bora.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news