Zanzibar imejikita zaidi kwenye kilimo cha viungo-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Zanzibar inajikita zaidi kwenye kilimo cha viungo (Spices) kutokana na sehemu kubwa ya uchumi wake kutegemea soko la utalii ambao unachangia asilimia kubwa ya uchumi wa nchi.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 18, 2024 Ikulu jijini Zanzibar alipozungumza na Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt. Gholamreza Nouri aliyefika na ujumbe wa wataalamu 15 kutoka sekta mbalimbali za maendeleo za nchi hiyo.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa, eneo muhimu litakaloimarisha ushirikiano wa diplomasia baina ya Tanzania na Iran hususani katika sekta ya kilimo.
Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi alimweleza mgeni wake huyo kuhusu kuzihuisha na kuziimarisha sehemu za historia katika kukuza soko la Utalii wa Urithi na kuboresha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania hasa Zanzibar na Iran kwenye eneo hilo la utalii. Rais Dk. Mwinyi amegusia Sekta ya Usafirishaji wa baharini na kuiomba Iran kuongeza ushirikiano kwenye eneo hilo ili kuimarisha biashara na uchumi kupitia bandari za pande mbili hizo kwa ushirikiano.
Kwa upande wake, Waziri Dkt. Gholamreza amesema watasaini makubaliano na Tanzania hasa Zanzibar kwenye sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo Kilimo, Utalii, Elimu,

Biashara na Sekta ya Uhandisi pamoja na kuahidi kutoa ushirikiano na kubadilishana uzoefu, mbinu na teknolojia kwenye maeneo hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news