Zanzibar itaendelea kuimarisha ushirikiano na Wakfu wa Qatar-Rais Dkt.Mwinyi

DOHA-Oktoba 30,2024 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa anamaliza ziara yake ya siku mbili nchini Qatar amekutana na Waziri wa Masuala ya Wakfu wa Qatar,Mheshimiwa Shanem bin Shaheem bin Ghaneem Ghanim.
Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Qatar kwa msaada mkubwa ilioutoa kufuatia janga la maporomoko ya udongo wilayani Hanang' mkoani Manyara mwaka 2023.

Mfuko wa Wakfu unaosimamiwa na Waziri huyo ulisaidia kwa kiasi kikubwa waathirika wa janga hilo.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema, angefarijika zaidi kuona kunaimarishwa ushirikiano baina ya pande mbili za Wakfu upande wa Zanzibar na Qatar.

Dkt. Mwinyi amemuomba waziri huyo kupitia mfuko wa Wakfu wa Qatar kuwasaidia wenzao wa Zanzibar kuwajengea uwezo hasa upande wa mafunzo ombi lililokubaliwa na Mheshimiwa Ghanem.

Rais Dkt.Mwinyi amemkaribisha Zanzibar Waziri huyo kujionea kazi za Wakfu zinavyofanyika.
Halikadhalika kuhusu Hijja, Dkt.Mwinyi alimuomba Waziri huyo kusaidia Mahujaji wa Zanzibar ambapo Zanzibar hupatiwa nafasi za Kuhiji elfu kumi na mbili kwa mwaka, lakini ni idadi ndogo tu ya mahujaji wanamudu kutekeleza nguzo hiyo muhimu ya Kiislamu.

Naye Waziri Ghanem amemuahidi Dkt. Mwinyi kulifanikisha suala hilo, kwani mwezi Januari mwakani atatembelea Saudia na na atazungumza nao namna ya kusaidia Mahujaji zaidi wa Zanzibar kushiriki Hijja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news