Zanzibar na Comoro zitaendeleza uhusiano wa kibiashara-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema wakati umefika wakurejesha diplomasia ya Uchumi na kuendeleza biashara baina ya Zanzibar na Comoro kwa maslahi ya pande zote mbili.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 9, 2024 Ikulu jijini Zanzibar alipozungumza na Gavana wa Jiji la Moroni, Visiwa vya Ngazija, Bw. Ibrahim Mzee aliyefika na ujumbe wake kuwasilisha dhamira ya kukuza ushirikiano baina nchi mbili hizo.
Pia,Rais Dkt. Mwinyi aliushauri ujumbe huo kurejesha makundi ya wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja Zanzibar kuangalia fursa za biashara na uwekezaji kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Amesema, ni vema kwa pande mbili hizo kufirikia namna ya kurejesha huduma ya usafiri wa vyombo vya baharini ili kuwanufaisha wananchi wa pande mbili hizo na fursa za biasahara na kijamii zilizopo.Halikadhalika, Dkt. Mwinyi ameshauri ujumbe huo kuweka utaratibu maalumu kwa walimu wa Zanzibar kwenda Comoro kufundisha Kiswahili au Wakomoro kuja Zanzibar kujifunza lugha hiyo jambo ambalo litakuwa na wepesi kwani lugha za nchini mbili hizi zinashabihiana.Kwa upande wake, Gavana Ibrahimu Mzee amesifu kasi ya mabadiliko na maendeleo makubwa ya Zanzibar na kusema kuwa nchi yake inakitu cha kujifunza kama ilivyofanikiwa Zanzibar.Vilevile alimualika Rais Dkt. Mwinyi kuzuru visiwa vya Ngazija kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye nyanja za maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news