Akiba Commercial Bank Plc yatoa msaada kwa waokoaji ghorofa lililoporomoka Kariakoo

DAR-Akiba Commercial Bank Plc imeendelea kujitoa si tu kuhudumia wateja wake bali pia kushiriki katika juhudi za kijamii wakati wa dharura na majanga, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kujenga jamii imara na yenye mshikamano.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Tobha Nguvira ambaye pia ni Msimamizi wa Kitengo cha Maafa Mkoa wa Dar es Salaam ameyasema hayo leo Novemba 17,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea msaada kutoka Akiba Commercial Bank Plc.
Ni walipofika kutembelea eneo la ajali la jengo la biashara lililoporomoka Kariakoo, ajali iliyosababisha madhara makubwa ikiwemo majeruhi, uharibifu wa mali na wengine kuangamia.

"Tunashukuru sana benki hii imetoa msaada wa katoni kadhaa za maji kwa ajili ya kusaidia timu ya uokozi inayofanya juhudi kubwa za kuokoa watu waliokumbwa na ajali hiyo mbaya na ya kusikitisha na wamekuja na Ujumbe wa Akiba Commercial Bank uliongozwa na wafanyakazi wa matawi ya Kariakoo pamoja na makao makuu akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Bi. Dora Saria na Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji, Dkt. Danford Muyango, amesema Dkt.Nguvira.
Naye Kaimu Afisa Biashara Mkuu, Dkt. Danford Muyango amesema, Akiba Commercial Bank Plc imewaomba wateja wake ambao wameathirika na janga la kuporomoka ghorofa Kariakoo kufika kwenye matawi kutoa taarifa za athari walizopata, kwani benki itatoa usaidizi wa tathmini wa kina kuhusu huduma za bima na kuanzisha utaratibu wa marejesho ya mikopo yao kulingana na hali yao.

Aidha, Akiba Commercial Bank imetoa pole kwa wale wote walioathirika, hivyo haitasita kutoa msaada wa kiutu pale utakapohitajika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news