Askari Magereza mbaroni kwa tuhuma za kumjeruhi mgombea wa CHADEMA kwa risasi

SINGIDA-Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia askari mmoja wa Jeshi la Magereza kwa tuhuma za kumjeruhi kwa risasi George Juma (41) ambaye ni mgombea wa kitongoji cha Stendi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Amon Kakwele amesema kupitia taarifa kwa umma kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Amefafanua kuwa, tukio hilo lilitokea jana Novemba 26 katika Kitongoji cha Stendi, Kata ya Mkwese Wilaya ya Manyoni mkoani Singida baada ya wafuasi wa CHADEMA kuvamia eneo ambalo wafuasi wa CCM walikuwa wakifanya kikao chao usiku.

“Baada ya uvamizi huo kulitokea vurugu na wenyeji wakapiga simu kwa askari hao ambao walikuwa karibu. Wakati askari magereza wakijaribu kuwasiliana na askari polisi wananchi ambao hawajajulikana walianza kurusha mawe.

“Askari hao waliamua kujihami kwa kupiga risasi hewani ambapo risasi moja ilimjeruhi George.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news