MORONI-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Umoja wa Visiwa vya Comoro, Mheshimiwa Azali Assoumani.
Mheshimiwa Rais Azali amemkabidhi Balozi Yakubu Ujumbe Maalum kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan na akielezwa kuridhishwa kwake na ushirikiano wa sekta za biashara na kijamii uliopo baina ya nchi hizo mbili.
Rais Azali pia alimueleza Balozi Yakubu kuwa ameshakutana na Marais wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi; Hayati Benjamin Mkapa; Mhe. Jakaya Kikwete; Hayati John Magufuli na sasa Rais Samia Suluhu Hassan na wote wameonesha upendo mkubwa kwa Comoro na anafurahi sasa kampuni za Tanzania zinakuja kuwekeza Comoro.