Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yazifungia Apps 69 zinazotoa mikopo mitandaoni

DAR-Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuwa imebaini kuwepo kwa Majukwaa na Programu Tumizi 'Applications” zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.
Aidha, Majukwaa na Programu hizo zimeshindwa kukidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 uliotolewa na Benki Kuu tarehe 27 Agosti, 2024 (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2 Microfinance Service Providers, 2024).

Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Hudumaza Fedha,ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, nautunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.

Kupitia taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu Umma kwamba Majukwaa na Programu Tumizi “Applications” zifuatazo hazina kibali na haziruhusiwi kuendelea na shughuli za utoaji mikopo kidijitali;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news