MUNICH-Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Halima Ramadhan Vunjabei ameshinda pambano lake kwa Knock Out ya raundi ya tatu.
Ni dhidi ya bondia Songul Ayten lililiofanyika usiku wa Novemba 23, 2024 mjini Munich nchini Ujerumani.
Halima Vunjabei anakuwa bondia wa kwanza mwanamke kushinda kwa KO nje ya nchi baada ya bondia Abdul Ubaya ambaye ni mwanaume kumchapa kwa KO bondia wa Urusi, Ibragim Estemirov.
Ubaya aliumana na Estemirov tarehe 25 Oktoba, 2024 na kuzawadiwa shilingi milioni tano kama zawadi ya Knock Out ya Mama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kutoa hamasa katika michezo mbalimbali nchini kwa muda mrefu sasa.