DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekutana na wadau wake kutoka benki za biashara na kujadiliana kuhusu zoezi la kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000) na elfu kumi (10000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003, na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010.
Kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 05 Novemba 2024 katika makao makuu ndogo ya Benki Kuu jijini Dar es Salaam, kimetoa fursa kwa washiriki kujadili kuhusu utekelezwaji wa zoezi hilo ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025 kupitia Ofisi zote za Benki Kuu na benki zote za biashara nchini.