BRELA yatoa taarifa kuhusu changamoto za Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao (ORS)

DAR-(Novemba 16, 2024)-Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inapenda kuutaarifu umma na wadau wote kuwa Mfumo wake wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) umepata changamoto ambazo zinakwamisha upatikanaji wa huduma zake kwa ufanisi unaotarajiwa.

Mfumo wa ORS umeunganishwa na Mifumo mingine ya Serikali ili kufanikisha sajili zake kwa njia ya mtandao. 

Inapotokea hitilafu katika moja wapo ya Mifumo ambayo ORS inaitegemea huathiri Mfumo wa usajili, hivyo kushindwa kuhudumia wateja wake kwa ufanisi.

BRELA inawahikishia kwamba wataalam wanaendelea na jitihada za kutatuachangamoto hizo ili kurejesha upatikanaji wa huduma kwa ufanisi. 

Wakala inaomba radhi kwa wateja wote kwa changamoto wanazozipata katika kupata huduma zake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news