CCM YASHINDA ASILIMIA 90.01 YA WENYEVITI WA VIJIJI

DODOMA-Katika maeneo yaliyofanya uchaguzi terehe 27 Novemba, 2024 kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji ni 12,271 kati ya nafasi 12,280 zilizopaswa kufanya uchaguzi. Kati ya nafasi hizo, CCM imeshinda nafasi 12,150 sawa na asilimia 99.01,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa ameyasema hayo usiku wa Novemba 28,2024 wakati akitangaza matokeo ya jumla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mohammed Mchengerwa.

CHADEMA imeshinda nafasi 97 sawa na asilimia 0.79, ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 sawa na asilimia 0.09, CUF imeshinda nafasi 10 sawa na asilimia 0.08, NCCR Mageuzi imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01,

UMD imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01 na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news