DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata ushindi wa viti 1,222 sawa na asilimia 0.53.
Ni katika nafasi ya wajumbe wa halmashauri za vijiji mbalimbali nchini huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiibuka na ushindi wa viti 229,075 sawa na asilimia 99.
Waziri Mchengerwa amesema hayo Novemba 28, 2024 wakati akitoa matokeo ya jumla ya uchaguzi huo.
Amesema,Chama cha ACT Wazalendo kimepata viti 232 sawa na asilimia 0.1, Chama cha Wananchi (CUF) kimepata viti 105, sawa na asilimia 0.05 na chama cha NCCR Mageuzi viti 16 sawa na asilimia 0.01.