CHAUMMA chapata mshindi mmoja wenyeviti wa mitaa

DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimepata kiti kimoja katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa wenyeviti wa mitaa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 27, 2024.
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashim Rungwe.

Amesema hayo Novemba 28, 2024 wakati akitoa matokeo ya jumla ya uchaguzi huo akikitaja Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuongoza kwa kupata jumla ya viti 4,213 sawa na asilimia 98.83 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikishika nafasi ya pili kwa kupata viti 36 sawa na asilimia 0.84.

Mapema akizungumzia kwa upande wa wenyeviti wa vijiji, Mchengerwa amesema huko pia CCM imeongoza asilimia 99.01 (viti 12,150) huku CHADEMA ikipata asilimia 0.79 (viti 97).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news