Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii,Dkt.Joyce Nyoni akipokea tuzo ya Uandaaji wa Taarifa za Hesabu za Kifedha katika Kundi la Vyuo vya Elimu ya Juu ambapo Chuo cha Ustawi wa Jamii kimeshika nafasi ya pili. Mkuu wa Chuo aliambatana na Mhasibu Mkuu Aisha Kapande, Wahasibu na wakaguzi wa hesabu za ndani kutoka Chuo cha Ustawi wa jamii.
Tuzo hizo zimetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) usiku wa tarehe 29/11/2024 APC Bunju jijini Dar es Salaam.