DAR-Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) yaharibu vifaa na bidhaa mbalimbali zilivyokamatwa katika operesheni za Uharamia wa kazi za ubunifu wa Sanaa na uandishi sambamba na urushaji wa matangazo kwa njia ya waya wa Kebo kama mpira na nyinginezo.
Akizungumza katika zoezi hilo Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki COSOTA Bi. Doreen Anthony Sinare alisema vifaa hivyo vilivyoharibiwa vinathamani ya kiasi cha milioni sabini na tano ila madhara ambayo yangesababishwa na vifaa hivyo pamoja na bidhaa hizo sokoni yangeweza kuwa makubwa zaidi ya kiasi hicho.
Zoezi hilo limefanyika Novemba 30, 2024 Jijini Dar es Salaam.
"Vifaa hivi vimekusanywa kutoka katika operesheni mbalimbali zilizofanyika na Ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Mtwara, Lindi, Pwani na kwingineko ikiwemo operesheni za urushaji wa matangazo kwa masafa ya Kebo kwa maudhui yasiyo na ruhusa kutoka kwa wamiliki na udurufu wa kazi za sanaa na uandiahi bila kibali cha wamiliki wa kazi hizo kama Filamu, Muziki na uchapishaji" alisema Doreen.
Pamoja na hayo Afisa Mtendaji Mkuu huyo alisema Uharamia unachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu kipato cha mbunifu ma serikali nani asiyefahamu sanaa na uandishi ni ajira, ni biashara na ni uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi? Anayejinufaisha kinyume na sheria ni kukosesesha hayo mambo matatu kwa nchi. Hivyo alitoa onyo kwa watu wote wanaofanya shughuli hizo kuacha mara moja.
Halikadhalika alitoa tangazo kuwa tayari COSOTA imepata taarifa za watu wanaosambaza kazi za Filamu kwa njia ya mtandao ikiwemo telegram na inaendelea kuchukua hatua ili kuhakikisha kuwa watu hao wanafikishwa katika vyombo vya Sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.