DCEA yang'ara tena katika usimamizi wa fedha za umma

DAR-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeendelea kung'ara katika uwanja wa usimamizi wa fedha za Umma.
Katika hafla ya tuzo iliyofanyika usiku wa tarehe 29 Novemba 2024,Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ilitangazwa DCEA kuwa mshindi wa kwanza tuzo ya umahiri katika utayarishaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2024 katika kipengele cha Taasisi za Serikali zinazojitegemea (independence government agency).
Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Kamishna Jenerali, Kamishna Hussein Mbanga alisema kuwa ushindi huu wa mara kwa mara unadhihirisha uadilifu wa DCEA katika kuhakikisha kuwa fedha za Umma zinazotumiwa katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya zinatumika kama inavyotakiwa.
Kwa upande wake, Mhasibu Mkuu wa DCEA, CPA Stephen J. Dalasi alisema kuwa ushindi huu ni ushahidi kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amepitisha kuwa hesabu za Mamlaka ni safi kabisa. Aliongeza kuwa utendaji huu bora utakuza zaidi imani ya Umma kwa DCEA katika usimamizi wa fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news