Dkt.Chang'a atunuku vyeti wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Mabadiliko ya Tabianchi nchini Monaco

MONACO-Dkt.Ladislaus Chang'a, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (Intergovernmental Panel on Climate Change-IPCC) amealikwa kuhudhuria na kutunuku Tuzo wakati wa Sherehe za 17 za Tuzo ya Kimataifa ya Afya ya Mfuko wa Mwana Mfalme Albert II wa Monaco (17th Planetary Health Awards Ceremony of the Prince Albert II of Monaco Foundation).

Wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu waliofaidika na mfuko huu wametunukiwa tuzo kwa kazi zao za utafiti ikiwa ni sehemu ya ushirikiano ulioanzishwa kati ya mfuko huo na IPCC.
Tukio hilo lenye hadhi kubwa katika tasnia ya sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi Duniani lilifanyika siku ya Alhamisi, 7 Novemba, 2024 katika ukumbi wa Opera Monte-Carlo, huko Monaco na kuongozwa na Mfalme Albert wa II wa Monaco.

Aidha, Dkt. Chang’a amekasimiwa pia na IPCC jukumu la kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Ufadhili wa Masomo wa IPCC (IPCC Scholarship Fund).

Hafla hii ya kutunuku vyeti aliyoshiriki Dkt. Chang’a ni heshima kwa Tanzania na Afrika, na imeendelea kuitangaza nchi yetu Kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news