Dkt.Faustine Ndugulile ametuachia simanzi kubwa-Spika Dkt.Tulia

MBEYA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amesema kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile, kimeacha simanzi kubwa kwa Bunge na Watanzania kwa ujumla kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taifa.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mtaa wa Uzunguni A jijini Mbeya leo Novemba 27, 2024, Dkt. Tulia amesema kuwa nyota ya Dkt. Ndugulile imezimika wakati akiwa ameanza kung’ara katika anga za kimataifa.

Alikuwa aanze rasmi majukumu yake mapya ya kimataifa mwezi Machi mwaka 2025.

Dkt. Tulia amesema kuwa Bunge limepoteza Mbunge mahiri ambaye pia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI. Mchango wake uliwezesha kufanikisha mabadiliko makubwa ya sheria na sera katika sekta za afya na mapambano dhidi ya UKIMWI.

Aidha, amewataka Wananchi wa Kigamboni kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho wamempoteza Mbunge wao na kumuombea apumzike kwa amani.

Dkt. Ndugulile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news