DAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt Natu El-maamry Mwamba amekutana na kufanya kikao na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mtaalamu Mwandamizi wa Maendeleo ya Jamii kutoka Benki hiyo, Bi. Claudia Zambra Taibo, pamoja na wataalamu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, Bw. Shedrack Mziray, katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN).
Tags
Benki ya Dunia Tanzania
Dr Natu El-maamry Mwamba
Habari
Picha
Picha Chaguo la Mhariri
Wizara ya Fedha Tanzania