DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Kampuni ya Black Rock Mining Limited, inayomiliki Kampuni Tanzu ya Faru Graphite, ukiongozwa na Mwenyeki wa Kampuni hiyo yenye Makao yake Makuu nchini Australia, Bw. Richard Crookes.
Mazungumzo hayo yalihusisha masuala ya utekelezaji wa Mradi wa Madini wa Mahenge Graphite uliopo mkoani Morogoro, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba alieleza umuhimu wa mradi huo katika maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii na kwamba Serikali itahakikisha kuwa mradi huo unafanyakazi kama ulivyokusudiwa.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu ya Faru Graphite, Bw. Ian Murray, Mkuu wa Masuala ya Fedha wa Kampuni ya Black Rock Mining Limited, Bw. Paul Sims, Meneja Uhusiano wa Kampuni Tanzu ya Faru, Bw. Alimiya Osman na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).