DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amezindua rasmi utoaji wa Hati Fungani ijulikanayo kama Bondi Yangu ya Benki ya Azania, inayotarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 100 kupitia soko la mitaji, hatua ambayo amesema ni kielelezo tosha cha umuhimu uliowekwa na Benki hiyo katika kukuza Sekta ya Fedha nchini. Tukio hilo limefanyika katika Hoteli ya Best Western jijini Dodoma.