WASHINGTON D.C-Mrepublicani Donald Trump ameshinda uchaguzi wa Rais wa Marekani ikiwa ni kwa wa vyombo vya habari Novemba 6,2024.
Julai, mwaka huu milio ya risasi ilisikika kwenye mkutano wa hadhara wa Donald Trump huko Pennsylvania wakati alipokuwa akitoa hotuba ambapo alikimbizwa nje ya jukwaa haraka na maafisa wa kitengo cha Secret Service. Ni jaribio ambalo lililenga kumuua.
Trump amemshinda Mdemokrasia Kamala Harris katika hali ya kushangaza ya kisiasa ambayo italeta mshtuko kote duniani.
Ushindi wa Mrepublican huyo mwenye utata, ukifuatia moja ya kampeni zenye uhasama zaidi katika historia ya kisasa ya Marekani, ulikuwa wa kushangaza zaidi ikizingatiwa msururu wa mashtaka yasiyo na kifani yaliyofunguliwa dhidi yake, jaribio la kuuawa, na onyo kutoka kwa mkuu wake wa zamani wa utumishi kwamba yeye ni "fashisti."
"Ni ushindi wa kisiasa ambao nchi yetu haijawahi kushuhudia hapo awali," Trump alisema katika sherehe ya ushindi huko Florida.
Makamu wa Rais Harris, ambaye aliingia kwenye kinyang'anyiro mnamo Julai baada ya Rais Joe Biden kusitisha kampeni yake, alifanya kampeni ya msimamo wa wastani iliyomulika ujumbe wa uchochezi wa Trump na matumizi ya mifano ya wazi ya ubaguzi wa rangi na jinsia.
Lakini onyo lake la kutisha kuhusu uhamiaji na kuunga mkono sera ya kujitenga viliweza kuwafikia wapiga kura walioathiriwa na athari za kiuchumi kufuatia janga la UVIKO-19, na wanaotaka mabadiliko kutokana na miaka ya Biden.
Kampeni ilionyesha kinyang'anyiro chenye ushindani mkali, lakini matokeo yalikuja kwa haraka sana, yakileta ushindi mzito ambao ulijumuisha ushindi katika majimbo muhimu ya Georgia, North Carolina, na Pennsylvania.
Trump ndiye rais wa kwanza zaidi ya karne moja kushinda muhula wa pili ambao si wa mfululizo.
Pia ndiye mtu pekee kuchaguliwa akiwa na kesi ya udanganyifu ambapo atakabiliwa na hukumu katika mahakama ya New York kwa udanganyifu mnamo Novemba 26.
Trump mwenye umri wa miaka 78, yuko katika njia ya kuvunja rekodi nyingine kama rais mzee zaidi aliyekalia kiti wakati wa kipindi chake cha miaka minne.
Atampita Joe Biden ambaye anatarajiwa kumaliza muhula wake Januari akiwa na umri wa miaka 82.
Hofu ya machafuko huko mbeleni
Thamani ya Dola ya Marekani iliongezeka huku sarafu ya mtandaoni ya bitcoin ikifikia kiwango cha rekodi na masoko mengi ya hisa yakiendelea kuongezeka, huku wafanyabiashara wakibashiri ushindi wa Trump kadri matokeo yalivyokuwa yanaingia. Lakini machafuko yanaweza kuwa mbele.
Ushindi wa Trump unakuja na ahadi yake ya mabadiliko makubwa ya sera, si tu nyumbani bali pia nje, ambapo msimamo wake wa kujitenga na sera ya "Marekani Kwanza" unatarajiwa kuwa na athari kubwa.
Amekuwa akionesha mara kwa mara kwamba angeweza kumaliza mzozo wa Ukraine kwa kuilazimisha Kyiv kukubali kutoa maeneo kwa Urusi, na tishio lake la kufukuza kwa wingi wahamiaji haramu limesababisha wasiwasi mkubwa katika bara la Amerika ya Kusini.
Aidha, anarejea Ikulu ya White House kama mkanushaji wa mabadiliko ya tabianchi, akiwa tayari kubomoa sera za kijani za mtangulizi wake Biden na kuweka hatarini juhudi za kimataifa za kupunguza joto linalosababishwa na binadamu.
Hata kabla ya ushindi wa kushangaza wa Trump kuthibitishwa kikamilifu, viongozi wa kigeni walikimbilia kutuma pongezi.
Miongoni mwao ni pamoja na washirika wa muda mrefu wa Trump, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye anatarajiwa kuona kupungua kwa haraka kwa msaada wa kijeshi kutoka Marekani mara Biden atakapondoka ofisini, alimtumia ujumbe wa pongezi Trump.Soma zaidi hapa》》》