Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Balozi wa Sri Lanka wajadili uwekezaji Sekta ya Fedha nchini

DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba leo  Novemba 26, 2024 amekutana na Balozi wa Sri Lanka nchini Tanzania mwenye makazi yake jijini Nairobi Kenya, ukiongozwa na balozi wake, Mhe. Kana Kananathan, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya fedha na uchumi kiujumla.
Akizungumza katika mkutano huo, Gavana Tutuba amesema Benki Kuu ya Tanzania inakaribisha wawekezaji kutoka Sri Lanka na nchi nyingine ulimwenguni kuwekeza katika sekta ya fedha kutokana na mazingira rafiki ya uwekezaji na utulivu wa sekta hiyo nchini.
Aidha, amesisitiza kuwa Benki Kuu imejizatiti kulinda mitaji ya wawekezaji pamoja na amana za wateja wa taasisi mbalimbali za fedha kupitia sheria na kanuni madhubuti zinazosimamia sekta hiyo.

Ameongeza kuwa,usimamizi mzuri wa sekta ya fedha hupelekea wawekezaji kupata faida bila kuwaumiza wateja wao na kuwekeza katika sekta nyingine za maendeleo.
Naye Balozi Kananathan, ameipongeza Benki Kuu kwa kusimamia vizuri uchumi nchi unaiofanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi rafiki kwa ajili uwezekaji. Pia, ameahidi kuendelea kushawishi wawekezaji kutoka nchi yake kuja Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news