Hawa ndio wakuu wa nchi na Serikalii wanawake waliowahi kushiriki Mkutano wa G20

RIO DE JANEIRO-Mkutano wa 19 wa kilele wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa kundi la nchi tajiri na zile zinazoinukia kiuchumi (G20) umefanyika jijini Rio De JJenairo nchini Brazil.
Katika mkutano huo wa Novemba 18 hadi 19,2024 ushiriki wa Tanzania kwa mara ya kwanza unatajwa kusaidia kupata fedha za masharti nafuu, na ushirikiano kwa ajili ya kupanua upatikanaji wa nishati safi.

G20 ambalo ni jukwaa la Kimataifa linalojumuisha mataifa makubwa ya kiuchumi duniani linaundwa na nchi wanachama 19 ikiwemo Argentina, Australia,

Brazil, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, India, Indonesia, Italia, Japan, Korea, Mexico, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Urusi, Türkiye (Uturuki), Uingereza na Marekani.

Sambamba na vyombo viwili vya Kikanda ambavyo ni Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya. Umoja wa Afrika umeshiriki katika mkutano huo kama mwanachama kwa mara ya kwanza tangu kukubaliwa kama mwanachama wa kundi hilo Septemba, 2023.

Wanachama wa G20 wanawakilisha karibu asilimia 85 ya Pato la Taifa la dunia, zaidi ya asilimia 75 ya biashara ya dunia na karibu theluthi mbili ya idadi ya watu duniani.

Awali, G20 ililenga zaidi masuala ya jumla ya kiuchumi, lakini ilipanua ajenda yake na kujumuisha masuala ya biashara, maendeleo endelevu, afya, kilimo, nishati, mazingira, mabadiliko ya tabianchi na mapambano dhidi ya rushwa.

Aidha, jukwaa hilo linajumuisha mawaziri wa fedha,magavana wa benki kuu, na pia marais au viongozi wa nchi husika na husaidia kuunda sera na mikakati ya kushughulikia changamoto hizo.

Hawa ndio wakuu wa nchi na Serikalii wanawake waliowahi kushiriki Mkutano wa G20;

Cristina Fernández de Kirchner

Huyu ni Rais Mstaafu wa Argentina aliyeshikilia nafasi hiyo kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2015.

Wakati wa uongozi wake ndipo Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi wa Kundi la G20 ulioanzishwa mwaka 1999 ulibadilishwa jina kutoka G8 hadi G20 mwaka 2008 na Rais Kircher kushiriki Mkutano wa G20 uliofanyika Pittsburgh, Marekani mwaka 2009.

Julia Gillard

Mkutano wa G20 wa mwaka 2010 ulifanyika jijini Seoul nchini katika Jamhuri ya Korea.

Waziri Mkuu wa Australia wa kipindi hicho naye alishiriki. Ifahamike kuwa kwa nchi ya Australia Waziri Mkuu ndio kiongozi wa ngazi ya juu zaidi ya nchi kama ilivyo Rais kwa nchi yetu. Mhe. Julia Gillard alihudumu kama Waziri Mkuu wa Australia mwaka 2010 hadi 2013 na bahati haimtupi mja, akiwa na siku 139 tu katika nafasi hiyo tangu aingie madarakani Juni 24, 2010, Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Australia alishiriki Mkutano wa G20 Seoul uliofanyika Novemba 11 na 12.

Lakini pia alishiriki mikutano ya G20 kwa mwaka 2011 Cannes, France, 2012 Los Cabos, Mexico, 2013 St. Petersburg, Russia na 2014 jijini Brisbane, Austral

Dilma Rousseff

Katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2016, mhe. Dilma Rousseff alihuduma kama Rais wa Brazil naye kama ilivyokuwa kwa Mhe. Gillard, katika kipindi cha kwanza cha uongozi wake aliweza kushiriki katika Mkutano wa G20 wa mwaka huo uliofanyika Ufaransa.

Kwa ujumla Mhe. Rousseff amewahi kushiriki mikutano mitatu ya G20, ikiwemo yam waka 2013 nchini Russia na 2014 nchini Australia.

Angela Markel

Mwanasiasa mkongwe na Kansela Mstaafu wa Ujerumani Angela Markel ndiye kiongozi aliyeweka historia hadi sasa ya kuhudhuria mikutano mingi zaidi ya G20 akiwa madarakani kati ya mwaka 2005 na 2021. Kansela Mkuu ndiyo nafasi ya juu zaidi nchini Ujerumani

Samia Suluhu Hassan

Nikirejea nyumbani, tofauti na viongozi hao wanne waliotangulia wote wanatoka katika nchi wanachama wa G20 hivyo kwa vyovyote vile vyeo vyao, tayari vinawapa nafasi ya kukeki katika mikutano hiyo tofauti na wale wanaoalikwa.

Mwaka huu 2024, Rais Samia Suluhu Hassan alipokea mwaliko wa kushiriki Mkutano wa G20 kutoka kwa Rais wa Brazil, Mhe. Luiz Inácio Lula da Silva na kuukubali mwaliko huo. Kushiriki kwake Mkutano huu wa 19 wa G20 kunamfanya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Afrika kualikwa kushiriki katika mkutano wa G20 na Rais wa kwanza wa Tanzania kushiriki Mkutano wa G20.

Kauli mbiu ya Mkutano wa Mwaka huu inayosema Building a Just World and a Sustainable Planet, yaani Kujenga jamii yenye haki, usawa na Maendeleo Endelevu pamoja na ajenda kuu za mkutano wa G20 Brasil katika kupambana na umaskini, njaa, mageuzi katika nishati na utunzaji wa mazingira vyatosha kuelezea kwanini mwaliko huu umeenda kwa mtu sahihi, kwani Rais Samia ni kinara namba moja katika kuyatekeleza haya ndani ya Tanzania.

Claudia Sheinbaum Pardo

Huyu ni Rais wa Mexico ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2018 hadi sasa. Katika Mkutano wa mwaka huu wa G20 Brasil, Rais Samia si Rais mwanamke pekee kwani Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum Pardo naye ameshiriki katika mkutano huu. Kwa mara ya kwanza Mhe. Pardo alishiriki mkutano huu akiwa Meya wa jiji la Mexico.

Kabla ya kufanywa kwa mageuzi na kuwa G20 mkutano huu ulijulikana kama G8 ukiwa na wanachama 8 tu Canada, France, Germany, Italy, Japan, Russia, Ulaya, na Marekani ambapo Marais wa Tanzania wa kipindi cha mwaka 2005 Hayati Benjamin Mkapa na mwaka 2008, Mhe. Jakaya Kikwete waliwahi kushiriki.

Wanachama wengine wa Kundi la G20 ni Canada, China, Ufaransa, India, Indonesia, Italy, Japan, jamhuri ya Korea, Mexico, Urusi, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Türkiye, Ulaya, Marekani, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news