ARUSHA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ametembelea Jengo la Ofisi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililoko jijini Arusha leo Novemba 21,2024.
Jengo liko katika hatua ya ujenzi na likikamilika litasaidia kusogeza huduma za Sheria kwa wananchi pamoja na vituo jumuishi ambapo jengo hilo litatoa huduma zote za kisheria kwa wananchi.
"Lengo letu ni kukamilisha ujenzi wa jengo hili na kurahisisha upatikanaji wa huduma za Kisheria kwa Wananchi husasani wa Jiji la Arusha na maeneo ya jirani,"amesema Mhe. Johari.
Katika hatua nyingine Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Jengo hilo mpaka kukamilika kwake litagharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 3 ambapo litaweza kuhudumia mikoa miwili, Arusha na Manyara hali itakayopelekea kufanya huduma hizo kusogezwa kwa ukaribu zaidi.