KILIMANJARO-Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Gervas Mgonja kwa madai ya kutoa kauli za kuhamasisha wananchi kuvamia makazi ya wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya kuonekana kwenye video mjongeo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii, akiwa anawahamasisha wananchi kufanya uhalifu huo Novemba 27,2024.