Karani jela miaka 22 kwa uhujumu uchumi na wizi wa ufuta

LINDI-Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi imemtia hatiani, Omari Ntauka kwa makosa ya uhujumu uchumi na kusababishia hasara ya shilingi 5,602,100 kwa kuiba kilogramu 1,855 za ufuta.
Ni alizokabidhiwa na wakulima katika tawi la Chilonji kwa msimu wa ufuta 2021/2022 kwa Chama cha Msingi cha Ushirika( AMCOS) cha Rweje.

Ilielezwa mahakamani hapo kwamba, mshtakiwa akiwa Karani wa Rweje AMCOS kwa makusudi alikisababishia hasara chama hicho cha msingi.

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi Na.21147/2024 ya Jamhuri dhidi ya Ntauka iliongozwa na Mhe. Neema Mhelela ambaye ni Hakimu Mkazi Mkuu na kusimamiwa na Wakili wa Serikali, Haruna Mchande wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Lindi.

Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu Novemba 11, 2024, Kosa la kwanza ni kuisababishia Hasara Mamlaka kinyume na Aya ya 10(1) ya Jedwali la Kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 marejeo ya mwaka 2022.

Kosa la pili ni wizi kinyume na kifungu cha 271 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022,

Mshtakiwa amehukumiwa kwenda jela miaka 22 ambapo katika kosa la kwanza adhabu yake ni miaka 20 na katika kosa la pili mshtakiwa amehukumiwa kwenda jela miaka miwili.

Adhabu hizo zinaenda sambamba na mshtakiwa kulipa hasara ya shilingi 5,602,100 aliyoisababisha kwa Chama hicho cha msingi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news