Katibu Mkuu Dkt.Shelukindo afanya mazungumzo na Mheshimiwa Boang

DAR-Katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 15 Novemba, 2024 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi, Dkt. Samwel Shelukindo alikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika inayosimamia masuala ya kibinadamu ambaye pia ni Balozi wa Botswana nchini Ethiopia, Mhe. Tebelelo Alfred Boang.
Kamati hiyo ilikuwa nchini ambapo pamoja na mambo mengine ilitembelea eneo la Hanang ambalo mwezi Desemba 2023 lilikumbwa na maporomoko ya ardhi na kusabisha vifo na uharibifu wa mali kwa wakati wa eneo hilo.

Kamati hiyo ilikabidhi msaada wa Dola 200,000 za Marekani kwa Ofisi ya Waziri Mkuu Maafa kufuatia janga hilo.

Akizungumza na ujumbe wa Kamati hiyo, Balozi Dkt. Shelukindo amemshukuru Mhe. Balozi Alfred na Umoja wa Afrika kwa mchango na misaada yao katika kukabiliana na majanga mbalimbali yaliyojitokeza nchini.

"Tumefurahi kupokea ujumbe huu kutoka Umoja wa Afrika baada ya Mvua kubwa, mafuriko na maporomoko yaliyoikumba na kuharibu Jamii yetu yaliyotokea Disemba 2023 na Aprili 2024."

Aidha,amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inakabiliana na majanga ya asili kwa kuhakisha tunaijenga Tanzania inayoweza kuhimili mabadiko ya tabia nchi.

Naye Mhe. Balozi Alfred amesema Umoja wa Afrika utaendelea kushirikiana kikamilifu na Tanzania na wadau wake na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na majanga ya asili pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikumba nchi.

"Tunaamini mshikamano ndio nyenzo imara ya kutatua na kukabiliana na changamoto mbalimbali."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news