Katibu Mkuu wa Utumishi afanya mazungumzo na bosi wa JICA

NA LUSUNGU HELELA

KATIBU Mkuu wa UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi kuhusu kuimarisha ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi kabla ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.

Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Miongoni mwa masuala waliyojadili ni pamoja na kutoa fursa za mafunzo kwa watumishi pamoja na maombi ya vibali vya ajira kwa raia wa kutoka Japan wanaokuja kufanya kazi nchini katika miradi ya Serikali katika Utumishi wa Umma ambapo fursa hiyo huwasaidia Wazawa kubaki na ujuzi unaoweza kutumika hata baada ya miradi ya maendeleo kukamilika
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akipeana mkono na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.
Aidha, viongozi hao wamepongeza juhudi za ushirikiano wa nchi hizo mbili unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Shigeru Ishiba.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan ( JICA), Bw. Ara Hitoshi mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya JICA na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora. Wengine ni Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na wageni waliombatana na Bw. Hitoshi.

Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu Mkuu Mkomi ameishukuru JICA kwa kuendelea kutoa ufadhili masomo wa elimu ya juu kwa Watanzania hususan watumishi wa umma huku akisisitiza kuwa ushirikiano baina pande mbili ni wa kihistoria na utaendelea kuimarika wakati wote katika masuala ya elimu na utumishi wa umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news