Lema adai Kigaila alihusika vurugu za Arusha, afichua siri nzito

ARUSHA-Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amedai vurugu zilizojitokeza juzi wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa chama Mkoa wa Arusha zilichochewa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Benson Kigaila.
Lema ameyabainisha hayo leo Novemba 16,2024 wakati akizungumza na wanahabari jijini Arusha.

"Hii ilikuwa ni organised crime kati ya watu wa CHADEMA na ndiyo maana na ninyi waandishi wa habari mlipatikana.Cha kusikitisha zaidi na hii ninaogopa kusema kwa sababu ninalisema, lakini ninaumia sana.

"Cha kusikitisha zaidi yale mambo mimi nilimuomba Naibu Katibu Mkuu Bara ateremke,Bw.Benson Kigaila...ateremke na nilimuomba ateremke awazuie wale wafanya fujo kwa sababu mmoja wa wafanya fujo ni rafiki yake mkubwa.

"Ambaye siku chache zilizopita alifanya fujo Monduli, mmoja wa wafanya fujo na alipofanya fujo Monduli mpaka uchaguzi wakamtukana msimamizi.

"Halafu wakati wakifanya fujo Monduli, mimi nilishuhudia kwamba, msimamizi alinipigia simu, nikamwabia afadhali hapa nipo na msimamizi wa uchaguzi Bw.Benson Kigaila unaweza ukaongea naye akasema hawa wanataka kunipiga.

"Wamepora na matokeo ya mabaraza,sasa sijui waliongea nini, lakini alisema kama uchaguzi wa wilaya haujatimia funga, halafu watu wa hamasa wakuondoe hapo muondoke.

"Kesho yake, mimi nikiwa na Benson Kigaila mmoja wa wafanya fujo akampigia simu, akaongea nae kama dakika 20.

"Niko na Benson, Moshi nikamwambia Benson, Naibu Katibu Mkuu Bara hawa watu wamefanya fujo, wamedhalilisha watu.

"Unapowapa audience ya kuongea nao na unapokuwa submissive kwao, alikuwa akiongea naye yeye akionekana kuwa mnyenyekevu kwao.

"Unatunyima sisi wengine mamlaka ya kichama, nikamwambia hii sio sawa sawa.

"Nikamwambia the ways unavyoongea na huyu Bwana hauongei sawa ni rafiki yake sana, Boni ni rafiki yake sana Benson Kigaila.

"Benson Kigaila akija hapa, anafikia kwa Boni na wakati mwingine wanatembea kwa pamoja, wanakula pamoja.

"Ni marafiki wa karibu sana,sasa nilipoona fujo zimechangamka na polisi wanataka kupanda ukumbini, mimi nilimuomba Naibu Katibu Mkuu ashuke chini, Naibu Katibu Mkuu ashuke chini amwambie rafiki yake asilete fujo.

"Naibu Katibu Mkuu...mtu wa kwanza, wa pili wa tatu baadaye nikatuma mtu mwingine nikasema kama hawezi kushuka nikamtuma Katibu wa Kanda, lakini ninaomba Naibu Katibu Mkuu ashuke chini.

"Baadaye alishuka, Naibu Katibu Mkuu alikuwa mgumu kuwafuata, nilimwambia wale ni rafiki zako, wafuate sisi hatuna mamlaka nao kwa sababu wewe una-communicate nao frequently.

"Mimi sina mamlaka, nimeshawaambia waondoke hapa, hawaondoki. Alitoa maelekezo ambayo kama yale maelekezo yangezingatiwa lazima ule uchaguzi ulikuwa unaharibika na polisi wangepanda juu kuondoa watu wote pale.

"Mimi niliwaambia vijana wetu wa hamasa...tumieni akili, watoeni pembeni bila kufanya jambo lolote lile.

"Naibu alirudi juu, aliporudi juu mimi niliendelea kuwasii polisi pale chini, nikawaambia tafadhali uchaguzi hauna muda mrefu sasa.Unaisha muda sio mrefu.

"Conclusion yangu ni nini? Huyu mmoja ambaye alikuwa anatukana sana ni rafiki sana na Naibu Katibu Mkuu Bara.

"Ni rafiki sana na Naibu Katibu Mkuu Bara, huyu aliyekuwa anatukana sana, lakini kinachonishangaza sana ni kwamba hata yule wa Ngorongoro aliyekuwa anatukana akisema kwamba... mimi nimekata majina yao.

"Sasa, hili jambo nitalisema kwamba mimi kwenye usaili huu maamuzi yoyote yakifanyika yanafanyika with collective responsibility.

"Lakini, mtu aliyeleta taarifa za Kuyaa, za tabia zake mbaya huko Ngorongoro, mbaya sana ni Naibu Katibu Mkuu Bara na akashawishi wajumbe kwamba huyu mtu hana sifa za kuwa kiongozi,"amedai Lema.

Hata hivyo, Lema amedai tayari ameagiza wote waliofanya fujo wachukuliwe hatua.

"Lakini, msimamo wa kwanza nimeagiza viongozi wa chama kanda mahali popote, kwa yeyote aliyehusika kwa sababu wako waliotoka Mkoa wa Kilimanjaro walikuja kufanya fujo Arusha.

"Kwamba taarifa ziende na wameziona hawa wanachama waliofanya huo upumbavu wa kiwango kile na kusababisha taharuki kubwa na udhalilishaji kwa chama chetu.

"Wachukuliwe hatua mara moja za kuvuliwa uanachama katika matawi yao mara moja na haraka iwezekanavyo,kwa sababu wamekidhalilisha chama sana,"ameongeza Lema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news