ZANZIBAR-Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar,Abubakar Lunda amefungua Mafunzo ya Maafisa Usalama Viwanjani, kutoka Vilabu vya Ligi Kuu ya Zanzibar pamoja na maafisa kutoka ZFF.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) yakiendeshwa na Mkufunzi N.S.S.O, Ramadhan Abdalla Bakari (Manyama) afisa anayetambuliwa na CAF ili kuwajengea uwezo Maafisa Usalama hao, kujua wajibu wao viwanjani.
Pamoja na mambo mengine, mafunzo hayo pia, yamezingatia suala la kulinda miundombinu ya viwanja vilivyotengenezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, inayoongozwa na Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi ili kuunga mkono juhudi zake katika kukuza michezo nchini.
Mafunzo hayo ni ya siku tatu yakianza Novemba 20,2024 na yatafungwa Novemba 23,2024.