DAR-Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni ameagiza Jeshi la Magereza kukaa na wataalam wa Wizara ya Ardhi na kamati ya urasimishaji, viongozi wa halmashauri na wananchi kuhakikisha wanayapima na kuyarasimisha maeneo ya wananchi yaliyokuwa na mgogoro na jeshi hilo, ametoa siku saba zoezi liwe limekamilika kama maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Masauni ametoa maagizo hayo alipofika katika eneo la Mazizini Kata ya Ukonga,Ilala jijini Dar Es Salaam ambapo kulikuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya wananchi na Jeshi la Magereza Ukonga.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo