PORT AU PRINCE-Baraza la Mpito nchini Haiti limemchagua, Alix Didier Fils- Aime kuwa Waziri Mkuu mpya nchini humo, baada ya baraza hilo kusaini amri ya kumfukuza Waziri Mkuu wa mpito, Garry Conille ambaye alishika nafasi hiyo kwa muda.
Baraza hilo liliteuliwa mwezi Aprili na kupewa jukumu la kumchagua waziri mkuu na baraza la mawaziri ambalo wanaamini linaweza kusaidia kutuliza mzozo nchini Haiti.
Hata hivyo, baraza hilo limekumbwa na mivutano ya kisiasa kwa baadhi ya wajumbe ambao wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo