DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema,aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango, marehemu Lawrance Mafuru alimuahidi kuondokana na tatizo la dola katika kipindi ambacho taifa ililipitia changamoto ya uhaba wa dola.
"Tulipopata changamoto ya dola ndani ya nchi niliunda kamati ikiongozwa na Mchechu akisaidiwa na Mafuru, na watendaji wengine kadhaa wa serikali, kamati ile ilifanya kazi kubwa na siku ya kufanya wasilisho mbele yangu kuweka mpango mezani wa kuleta dola ndani ya nchi Mafuru aliniambia Mheshimiwa tukiufuata mpango huu kama tulivyouleta nchi itaondokana na tatizo hili sio muda mrefu
“Leo wote ni mashahidi badala ya kuzibembeleza benki zitupe dola sasa benki zinatuita tukachukue dola kwao, lakini badala ya kulalamika nchi haina dola nimesikia juzi wazalishaji wanalalamika nchi haina shilingi,” amesema Rais Samia.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo