TABORA-Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Sagali Masanja (62) mkazi wa Kijiji cha Mahene, wilayani Nzega kisha kumkata titi na sehemu za siri na kuondoka navyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Richard Abwao, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi, saa 7:00 usiku, huku chanzo kikitajwa ni imani za kishirikina.
Alisema, watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya mauaji ya bibi huyo wakimtuhumu kuwa mchawi akidaiwa kuhusika na tukio la kumloga mtoto aliyefia kisimani.
Kamanda Abwao alisema, bibi huyo aliuawa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili kisha wauaji kuondoka na titi moja, sehemu zake za siri na pia kuchukua begi lake la nguo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo