NAIROBI-Aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya, Prof. Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa Naibu Rais mpya wa Kenya akichukua nafasi ya Rigathi Gachagua ambaye aliondolewa madarakani, huku akiapa kuwa mtiifu kwa rais na kumshukuru Dkt. William Ruto kwa kumuamini.
Novemba 1,2024 akihutubia katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi muda mfupi baada ya kuapishwa, Prof. Kindiki amesema,atahudumu nafasi hiyo kwa kumsaidia Rais kuongoza Taifa la Kenya na kuwashukuru wale wote waliochangia mafanikio yake.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo