MARA- Watu tisa wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba walizokuwa wakiishi kusombwa na maji baada ya mto uliopo jirani na makazi yao kujaa maji, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Tarime.



Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Edward Gowele amesema hadi sasa miili saba imekwishaopolewa kutoka mtoni na utafutaji wa miili mingine unaendelea kwa kushirikisha vyombo vya uokoaji na wenyeji wa eneo hilo.

Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo