MTWARA-Watu 23 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la shule ya msingi ya Salem kugongana na gari ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) eneo la Migomigo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.
Ajali hiyo imetokea Novemba 29,2024 majira ya saa 12 jioni katika eneo hilo la Migomigo barabara ya kutoka Newala mkoani humo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula, Zawadi Bwanali amethibitisha kuwapokea majeruhi hao 23 wa ajali hiyo ambapo kati ya hao wanafunzi ni 20, walimu wawili pamoja na dereva mmoja.