KIGOMA-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo Novemba 6, 2024 ameshiriki maziko ya marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Emmanuel Tutuba yaliyofanyika kijijini kwake Kibondo mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (B0T) Emmanuel Tutuba alipowasili wilayani Kibondo mkoani Kigoma kushiriki maziko leo.
Maziko hayo yametanguliwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu wilayani Kibondo na kuongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Mhashamu Askofu Joseph Mlola.
Akitoa salamu za rambirambi, Makamu wa Rais amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali nzima wanaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada ya kuaga mwili wa marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Emmanuel Tutuba iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu Kibondo mkoani Kigoma tarehe 06 Novemba 2024.




Amesema pia aliwatunza vyema watoto wake katika maadili na kuhakikisha wanapata elimu na hivyo kutumika kulisaidia Taifa.
Ametoa wito kwa wazazi na walezi kujenga tabia ya kuhakikisha watoto wao wanapata elimu itakayowasaidia wao na Taifa kwa ujumla.
Aidha amewasihi watanzania kutimiza wajibu wao katika jamii ikiwemo kuwaenzi na kuwatunza wazazi na walezi wao pindi wanapohitaji msaada.
Makamu wa Rais ametoa wito wa kuwajenga watoto katika maadili mema yatakayoanzia katika imani za dini.