DAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Ismail Samamba amewataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuweka nguvu kwenye usimamizi wa usalama na mazingira kwenye migodi ya madini hasa katika msimu huu wa mvua ili kuepuka ajali zinazoweza kutokea na kusababisha vifo.


Katika hatua nyingine,amewapongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwa mwenendo bora wa ukusanyaji wa maduhuli na kuwataka kuendelea kuwa wabunifu ikiwa ni pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.


Aidha, amewataka kuendelea kusimamia kwa karibu watumishi waliopo chini yao na kusisitiza kuwa Wizara ya Madini itaendelea kutatua changamoto ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kutosha na uboreshaji wa maslahi ya watumishi.